Psalms 11

Kumtumaini Bwana

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 aKwa Bwana ninakimbilia,
unawezaje basi kuniambia:
“Ruka kama ndege kwenye mlima wako.
2 bHebu tazama, waovu wanapinda pinde zao,
huweka mishale kwenye uzi wake,
wakiwa gizani ili kuwapiga
wale wanyofu wa moyo.
3 cWakati misingi imeharibiwa,
mwenye haki anaweza kufanya nini?”

4 d Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu;
Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.
Huwaangalia wana wa watu,
macho yake yanawajaribu.
5 e Bwana huwajaribu wenye haki,
lakini waovu na wanaopenda jeuri,
nafsi yake huwachukia.
6 fAtawanyeshea waovu makaa ya moto mkali
na kiberiti kinachowaka,
upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

7 gKwa kuwa Bwana ni mwenye haki,
yeye hupenda haki.
Wanyofu watauona uso wake.
Copyright information for SwhNEN